Faragha kwa Mpanda Kanisa ni mpango wa mafunzo kwa mpanda Kanisa kufikiri juu ya vidokezo muhimu vya kuanzisha jamii mpya ya imani. Mara nyingi huendeshwa kwa siku mbili au tatu,wapanda Kanisa,mara nyingine na wenzi wao,watatafakari vidokezo kumi tofauti kuhusiana na kuanzisha kituo kipya cha ufalme. Muda wa pamoja sio tu kwa ajili yaliyomo kwenye vipindi,bali ni kujifunza kila mtu kwa mwenzake, kutumia muda kwa maombi na marejeo na kuisikiliza sauti ya Mungu.
Warsha hii huwasidia viongozi kufikiri juu ya kazi na uwezo ulio wa lazima kupanda Makanisa yenye afya. Inahusisha mada kama vile msingi wa kibiblia katika upandaji wa Kanisa, maelezo mafupi na familia ya mpanda Kanisa, hatua za upandaji wa makanisa, mitindo ya upandaji wa Kanisa na sifa za kanisa lenye afya.
Warsha ya kuimarisha Kanisa lako huwawezesha Viongozi wa Kanisa kuliweka kusanyiko kwenye lengo la kazi yake kama wakala wa Mungu katika eneo husika. Warsha inatoa umuhimu wa maono yanayoelezeka kibiblia, inawaongoza kwenye tabia kumi za Kanisa lenye afya, na inawavuta Viongozi kuliona Kanisa lao kama mfumo unaoweza kuwa na matokeo muhimu katika jamii yake.
Karibu katika ulimwengu wa malezi. Katika warsha hii yenye vipindi vinne, utapata misingi ya mpango wa malezi inavyopaswa kuwa. Ijapokuwa vile vinavyofundishwa katika vipindi hivi vinne vinaweza kutumiwa katika muktadha mbalimbali ndani ya Kanisa, kusudi la mafunzo haya maalum ya malezi ni kwa wale watakaowaelekeza wapanda Kanisa walio kwenye mafunzo.
MAELEKEZO YA KUZINGATIA: Kitabu cha Mshiriki kina nafasi zilizo wazi kwa ajili ya kila neno lililopigiwa mstari katika kitabu cha mwezeshaji. Majibu yameorodheshwa chini ya ukurasa wa kitabu cha somo. (Maelekezo haya hayapo kwenye toleo la pdf la kitabu hiki).
You'll receive monthly updates on what God is doing through all of us together around the world.