Faragha kwa Mpanda Kanisa ni mpango wa mafunzo kwa mpanda Kanisa kufikiri juu ya vidokezo muhimu vya kuanzisha jamii mpya ya imani. Mara nyingi huendeshwa kwa siku mbili au tatu,wapanda Kanisa,mara nyingine na wenzi wao,watatafakari vidokezo kumi tofauti kuhusiana na kuanzisha kituo kipya cha ufalme. Muda wa pamoja sio tu kwa ajili yaliyomo kwenye vipindi,bali ni kujifunza kila mtu kwa mwenzake, kutumia muda kwa maombi na marejeo na kuisikiliza sauti ya Mungu.