Karibu katika ulimwengu wa malezi. Katika warsha hii yenye vipindi vinne, utapata misingi ya mpango wa malezi inavyopaswa kuwa. Ijapokuwa vile vinavyofundishwa katika vipindi hivi vinne vinaweza kutumiwa katika muktadha mbalimbali ndani ya Kanisa, kusudi la mafunzo haya maalum ya malezi ni kwa wale watakaowaelekeza wapanda Kanisa walio kwenye mafunzo.