Warsha ya kuimarisha Kanisa lako huwawezesha Viongozi wa Kanisa kuliweka kusanyiko kwenye lengo la kazi yake kama wakala wa Mungu katika eneo husika. Warsha inatoa umuhimu wa maono yanayoelezeka kibiblia, inawaongoza kwenye tabia kumi za Kanisa lenye afya, na inawavuta Viongozi kuliona Kanisa lao kama mfumo unaoweza kuwa na matokeo muhimu katika jamii yake.